ZANZIREE

с понедельник, июня 24, 2019 - 09:00 по пятница, июня 28, 2019 - 16:00
Point с центром широты -6.2093384 и долготы 39.2128672.

 

Chama cha Skauti Tanzania kinayo furaha kutangaza maadhimisho ya Jamboree ya Skauti Zanzibar (1912 – 2019) baada ya maadhimisho ya Miaka Mia (100) ya Skauti Tanzania Bara toka kianzishwe mwaka 1917 – 2017. Huu ni umri mkubwa unaostahili kusherehekea kama sehemu ya kufanya tathmini na kuona jinsi tutakavyopiga hatua kwenda mbele. Maadhimisho haya yatawahusu Skauti wote pamoja na wadau wake wa ndani na nje ya nchi, ambao watakaoshiriki watalazimika kualikwa na kuthibitisha ushiriki wao mapema iwezekanavyo.

 

Katika kilele cha maadhimisho ya Miaka 100 ya Chama cha Skauti Tanzania, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd aliagiza sherehe hizi zifanyike Mwaka 2019 Visiwani Zanzibar. Chama kimezingatia agizo hili na kulitekeleza. Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais iliwasilisha pendekezo hilo kupitia Baraza la Mapinduzi kupitia kikao cha Tarehe 31 Desemba, 2018 ilijadili na kuidhinisha kufanyika kwa maadhimisho haya Tarehe 24 – 28 Juni, 2019. Pamoja na mambo mengine Baraza liliagiza Ofisi ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali kuratibu mchakato mzima wa maandalizi kwa kuunda Timu ya Taifa ya kushughulikia suala hili ambapo kazi hiyo ilishafanyika na vikao vinaendelea. Vile vile Baraza liliagiza Wizara ya Elimu kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kuagiza kila Halmashauri kufadhili skauti 24 ili waweze kushiriki Maadhimisho husika. Eneo la Maadhimisho litakuwa Viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

2. AGIZO LA KAMISHNA MKUU
Kila Mkoa utatakiwa kushiriki kwa kutuma Skauti angalau Kumi (10) au zaidi. Tunakaribisha washiriki wa ngazi (section) ya Kabu, Junia, Sinia hadi Rova. Kila mshiriki anawajibika kujigharamia usafiri na matumizi mengine awapo safarini. Ada ya ushiriki itagharamia mahitaji ya msingi pindi mshiriki awapo Kambini. Kila Kiongozi wa Kundi anawajibika na usimamizi wa watoto/Vijana kwa kuhakikisha wanasafirishwa hadi Unguja na kurudishwa. Fedha za ada Tsh 80,000/= kwa kila mshiriki zitalipwa kwenye akaunti iliyopo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

 

1) Kamishna wa Mkoa na Kamishna wa Wilaya muwatangazie na kuwashawishi wahusika wakiwemo wajumbe wa Kamati zenu za Uendeshaji, Wajumbe wa Kamati zenu za Utendaji, Wajumbe wa
Mabaraza yenu na wapenzi wa Skauti. Taratibu nyingine za kufanikisha hili kwa ubunifu chanya zinabaki kwenu kwa mahusiano mazuri mlionayo na wadau wenu.
2) Kwa mujibu wa Sera ya Ulinzi wa Watoto na Vijana ya Chama cha Skauti Tanzania (Ibara 2.0 1) imeeleza kuwa katika kambi zote za kurejea kwa siku na za kulala ni lazima uwepo usimamizi wa watu wazima wawili ambao ni viongozi. Viongozi wawili watakuwa ni wavaa sare mmoja mwanamume na mwingine mwanamke.

3) Kila Kamishna wa Mkoa ahakikishe anaandaa vijana kushiriki katika maonyesho ya shughuli za Skauti zinazohusu Mkoa husika mfano: Ujasiria mali, Utamaduni, kilimo, ufundi stadi, Huduma ya Kwanza, Ujasiri n.k.

**Makamishna wa Skauti Mikoa ya Zanzibar wanahimizwa kuandaa shughuli za ubunifu kwa utaratibu rasmi na kuwasilisha mipango kazi yao kwenye Kamati kuu ya Maandalizi kwa ajili ya kuingizwa kwenye ratiba na kufanyiwa ukaguzi wa awali.

3. TAREHE YA MWISHO YA KUTHIBITISHA USHIRIKI
Makamishna wote wa Mikoa mnatakiwa kuthibitisha ushiriki wenu pamoja na ujumbe wenu ifikapo tarehe 10/06/2019. Hii ni kwa ajili ya kusaidia masuala ya maandalizi huko Zanzibar ikiwemo suala la malazi, chakula na mengineyo.

 

Utaratibu wa Malazi:
Mahema (yatatolewa na Serikali) iwapo utakuwa na ‘tent’ binafsi ni vyema sana ukaja nalo kwani litakupa wepesi michakato ya kambini.

 

Eneo la Kambi: Viwanja vya Maisara, Wilaya ya Mjini

4. UTARATIBU WA MALIPO
Fedha zote za ada ya ushiriki zitumwe kwenye akaunti ya Ifuatayo:
Jina la Akaunti: Tanzania Scouts Association
Jina la Benki: NMB Benki, Tawi la Zanzibar
Akaunti Namba : 22910032514
*Tafadhali tunza risiti yako ya benki uliyolipia kwani utaitumia kama tiketi ya kuingia kambini

 

5.HITIMISHO

Ndugu viongozi, ni inazidi kuwasisitiza kuhusu ushiriki we etu kwa wingi kwenye maadhimisho haya a kwa kuwa tunatarajia Mgeni rasmi ssiku ya Ufunguzi kuwa Mlezi wa Chama ccha Skauti Tanzania kwa upande wa VVisiwani, Mheshimiwa Dr. Mohamed Ali i Shein, Rais wa Serikali ya Mapin nduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa BBaraza la Mapinduzi. Uzinduzi wa MMaadhimisho haya ya Kihistoria unataraji iwa kuwa tarehe 25/06/2019.

 

Asanteni na nawata akia wote maandalizi mema.

 
Grace Kado
KAMISHNA MKUU

 

 

 

 

Updates

There are no updates for this event

You should not see this

Комментарии

Аватар пользователя jumbe311

tutakuwa pamoja mwenyezi mungu ajaliapo

Аватар пользователя Paul Andrew

Bravooo am Paul from Kenya at a place called Embu county youth leader en hope to attend

Аватар пользователя Tanzania Scouts Association
from Tanzania, United Republic of, 6 месяцев назад

Тип события

National

Organizers

Теги

For More Information, Please Contact;

National Executive Commissioner
Tanzania Scouts Association
P.O. BOX. 945
DAR ES SALAAM,

TEL: +255 222 153342 FAX: + 255 222 124807 EMAIL: tscouts2002@gmail.com
Mobile: +255 715 009 618 | +255 686 600 618 Email: eline.kitaly@yahoo.com

Topics

Youth Programme

SDG

Are you sure you want to delete this?
Welcome to Scout.org! We use cookies on this website to enhance your experience.To learn more about our Cookies Policy go here!
By continuing to use our website, you are giving us your consent to use cookies.