Kuanzia tarehe 11 hadi 16 Desemba 2016 kutakuwa na Shuguli za Skauti za Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Jukwaa la Vijana, Mashindano na Kikao cha Makamishna Wakuu mkoani Arusha kwa lengo la kuwakutanisha Skauti pamoja na ili waweze kubadilishana stadi

Kuanzia tarehe 11 hadi 16 Desemba 2016 kutakuwa na Shuguli za Skauti za Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Jukwaa la Vijana, Mashindano na Kikao cha Makamishna Wakuu mkoani Arusha kwa lengo la kuwakutanisha Skauti pamoja na ili waweze kubadilishana stadi za Skauti kwa nchi hizo za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani Kusini na Ethiopia. Kwa taarifa hii, Makamishna na Viongozi wa Makundi mnaombwa kuzingatia yafuatayo: Kwa Kila kiongozi atakayehitaji Skauti wake waweze kushiriki atume idadi kamili ya washiriki Watazamaji (Observers) ili yatumwe kwenye kamati ya Maandalizi ya Afrika Mashariki kwani tuna nafasi 200 tu. Kila Skauti 10 wataongozana na Kiongozi mmoja (1) tu na watalipia kiasi cha Tshs: 150,000/= ambayo ni sawa na Tshs 15,000/= kwa kila Skauti mmoja. Pamoja na malipo hayo Skauti wako watajitegemea kwa Usafiri, malazi na chakula.Kila mkoa umepewa nafasi 10 tu. Ushiriki wa Jukwaa la Vijana (Youth Forum) ni Tshs 70,000/= kwa kila Rova. Idadi ya Rova watazamaji wa YF ni nne (4) tu kwa kila nchi, hivyo wahi nafasi ni chache mno. Tuma ada kupitia akaunti namba: 20910006475 NMB, TANZANIA SCOUTS ASSOCIATION. Kwa maelezo namaswali zaidi wasiliana na Kamishna Mkuu Msadizi Program za Vijana 0655756688 (xyzohama@yahoo.com) au kamishna Mtendaji 0715009618 (tscouts2002@gmail.com).
Avatar Murtadhwa El Bahsan
from Tanzania, United Republic of, 5 tahun yang lalu
Are you sure you want to delete this?
Welcome to Scout.org! We use cookies on this website to enhance your experience.To learn more about our Cookies Policy go here!
By continuing to use our website, you are giving us your consent to use cookies.