TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)

JAMBOREE YA HEWANI YA SKAUTI YA KIMATAIFA KUFANYIKA KITAIFA BARIADI MKOANI SIMI YU TAREHE 15 NA 16 OKTOBA 2016.

Jamboree ya Hewani ya Skauti ya Kimataifa (World Scouts Jamboree On The Air) itafanyika Kitaifa Bariadi mkoani Simiyu tarehe 15 na 16 Oktoba 2016.

Jamboree ya Hewani ya Skauti ya Kimataifa ni Jamboree inayo waunganisha skauti wote duniani kwa kutumia vifaa vya Mawasiliano ya Radio (Radio calls) pamoja na Mtandao wa Intanet maarufu kama JOTA-JOTI.

Madhumuni ya Jamboree hii ni kuwaweka karibu skauti wote duniani kwa kutumia Teknolojia ya kisasa ya Mawasiliano na pia skauti pote duniani hujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kubadilishana taarifa na mafunzo mbalimbali ya Kiskauti.

Jamboree ya Hewani ya Kimataifa ya Skauti ni shughuli ambayo hufanyika Kitaifa kila mwaka mwezi wa Oktoba chini ya Uratibu wa Makao Makuu ya Chama cha Skauti Tanzania.

Jamboree hii pia hufanyika kwa kubadilishana mkoa kwa mkoa na mwaka huu 2016 Skauti wa Mkoa Simiyu wamepewa Heshima ya kuwa Wenyeji wa Maadhimisho hayo.

Jamboree ya Hewani ya Kimataifa ya Skauti inafanyika sambamba na wiki ya Taifa ya Vijana pamoja na Maadhimisho ya Siku ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambayo imeanza tarehe 7 na kufikia kilele chake tarehe 14 Oktoba 2016.

Skauti kutoka mkoa wa Mkoa wa Simiyu na wilaya zake pamoja na wengine kutoka mikoa ya jirani ya Mwanza, Shinyanga, Tabora, Mara na D’salaam wapo mkoani Simiyu tangu mwanzo wa Wiki ya Vijana Kitaifa tarehe 7 Oktoba 2016 hadi tarehe 16 Oktoba 2016 itakapofungwa rasmi kambi hiyo

Jamboree ya Hewani ya Kimataifa ya Skauti inafanyika katika eneo la shule ya Sekondari ya Bariadi na inatarajiwa kufunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu siku ya Jumamosi tarehe 15 Oktoba 2016.

Jumla ya skauti zaidi ya 500 wanatarajia kuhudhuria Kambi hii ya Kimataifa ya Jamboree ya Hewani ya Kiskauti.

KAULI MBIU – DUNIA NI YAKO – THE EARTH IS YOURS...

Avatar Tanzania Scouts Association
from Tanzania, United Republic of, 3 tahun yang lalu
Are you sure you want to delete this?
Welcome to Scout.org! We use cookies on this website to enhance your experience.To learn more about our Cookies Policy go here!
By continuing to use our website, you are giving us your consent to use cookies.